Home Dauda TV Video: Ripoti ya daktari kuhusu hali ya Mbaraka Yusuph anaetibiwa Afrika Kusini

Video: Ripoti ya daktari kuhusu hali ya Mbaraka Yusuph anaetibiwa Afrika Kusini

6732
0
SHARE

Daktari wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ametaja wachezaji watatu ambao wamepumzishwa kutoka kwenye kikosi ch Stars kutokana na majeraha waliyoyapata nchini Afrika Kusini kwenye michuano ya COSAFA Cup 2017.

Benno Kakolanya, Shabani Idd na Mbaraka Yusuph ni wachezaji ambao hawatakuwepo kwenye kikosi cha Tanzania ambacho kitacheza mechi dhi ya Rwanda kuwania kufuzu kucheza fainali za CHAN.

Kati ya hao watatu, Mbaraka Yusuph anatajwa kuwa na tatizo kubwa ukilinganisha na wengine, mshambuliaji huyo amefanyiwa upasuaji wa goti na atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa wiki nne hadi sita.

Mbaraka ameachwa Afrika Kusini ili kuendelea na matibabu wakati timu ya Taifa iliposafiri kurejea nyumbani kwa ajili ya mechi dhidi ya Rwanda itakayochezwa Julai 15, 2017 kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here