Home Kitaifa Video: Dylan Kerr amezungumzia mechi ya Everton, hakuacha kuitaja klabu yake ya...

Video: Dylan Kerr amezungumzia mechi ya Everton, hakuacha kuitaja klabu yake ya zamani Simba

10186
0
SHARE

Kocha wa zamani wa Simba Dylan Kerr amekuja kwa mara nyingine Tanzania lakini safari hii akiwa ni kocha wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya ambao Julai 13, 2017 watacheza mechi ya kirafiki vs Everton ambao wanakuja nchini kwenye ziara yao ya pre-season.

Ujio wa timu Everton umesimamiwa na SportPesa ambao pia ni wadhamini wa timu hiyo pamoja na Gor Mahia ambao wamepata fursa hiyo baada ya kuwa washindi wa SportPesa Super Cup 2017 mashindano ambayo yalishirikisha vilabu vyote vinavyodhaminiwa na SportPesa kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Kerr hakuacha pia kuizungumzia klabu yake ya zamani Simba ambapo amesema ame-miss mashabiki wa klabu hiyo pamoja na maisha mengine nje ya uwanja.

Katika kikosi cha Gor Mahia kuna mchezaji Jean-Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ aliyewahi kucheza Azam FC pia amezhungumzia matarajio yake kuelekea mechi dhidi ya Everton.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here