Home Kimataifa Tetesi za usajili barani Ulaya

Tetesi za usajili barani Ulaya

11672
0
SHARE

Tayari kiungo wa klabu ya Fc Monaco Tiemoue Bakayoko ameondoka Ufaransa na taarifa zinasema ameelekea Uingereza kusaini Chelsea lakini Manchester United inasemekana wanajaribu kuharibu dili hilo.

Matumaini ya kocha Pep Gurdiola kumsajili mlinzi wa kulia wa Juventus Dani Alves yanaonekana kuzimwa kwani beki huyo yuko njiani kujiunga na klabu ya Ufaransa ya PSG ambapo wanatarajia kumsainisha rasmi ndani ya saa 24 zijazo.

Baada ya kupoteza namba ya kudumu katika kikosi cha Mamchester United sasa mshambuliaji kwa klabu ya Manchester United Anthony Martial anaweza kuhamia katika klabu ya As Roma kwa mkopo wa muda mrefu.

Baada ya klabu za Chelsea,Man City na Liverpool kuonekana kusuasua katika usajili wa mlinzi wa Southampton Virgil Van Dijk sasa klabu ya Arsenal nayo imeingilia kati usajili huo na wanataka kumshawishi kujiunga nayo.

Baada ya kimnunua Romelu Lukaku kutoka Everton sasa klabu ya Manchestet United imejipanga kutuma ofa ya £60m kwa ajili ya kumnunua kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspur Eric Dier.

Klabu ya Tottenham Hotspur nayo imeingia vitani kumsajili kinda wa klabu ya Man City Kilechi Iheanacho ambaye yuko njiani kuondoka klabuni hapo huku klabu mbali mbali ikiwemo Leicestet City zikitajwa kumhitaji Mnigeria huyo.

Baada ya mvutano wa muda sasa kati ya Ac Millan na wakala wa golikipa wao Gianluigi/Gigi Donarruma sasa golikipa huyo amesaini mkataba mpya katika klabu hiyo utakaombakisha hadi mwaka 2021.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here