Home Kitaifa Picha 6: Gor Mahia walivyoingia Dar kuikabili Everton ya England

Picha 6: Gor Mahia walivyoingia Dar kuikabili Everton ya England

3104
0
SHARE

Kikosi cha wachezaji wa Gor Mahia tayari kimewasili Tanzania kwa ajili ya mchezo dhidi ya Everton siku ya Alhamisi Julai 13, 2017 kwenye uwanja wa taifa.

Gor Mahia wamewasili wakiwa na kocha wao mpya Dylan Kerr ambaye aliwahi kuwa kocha wa Simba kabla ya kufukuzwa baada ya timu yake kutolewa mapema kwenye muchuano ya Mapinduzi Cup Zanzibar Januari 2016.

Utakumbuka kwamba, Gor Mahia ndio washindi wa michuano ya SportsPesa Super Cup 2017. Taji hilo ndio limewapa Gor Mahia tiketi ya kucheza na Everton ambao pia wanadhaminiwa na kampuni ya SportPesa.

Kitu cha kipekee kwenye mechi ya Alhamisi kati ya Gor Mahia dhidi ya Everton ni uwepo wa nyota Wayne Rooney ambaye amesaini hivi karibuni kujiunga na wakali hao wa England na kuthibitisha ujio wa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United.

Everton inatarajia kuwasili kesho ikiwa na kikosi chote cha wachezaji watakaocheza msimu ujao kwenye ligi kuu England.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here