Home Kimataifa Novak Djokovic atinga robo fainali Wimbledon

Novak Djokovic atinga robo fainali Wimbledon

1904
0
SHARE

Baada ya Rafael Nadal kuoneshwa mlango wa kutokea katika michuano ya Wimbledon hapo jana, hii leo Novak Djokovic naye alikuwa uwanjani kuonesha nini anaweza kufanya.

Novak Djokovic alikuwa akikabiliana na Mfaransa Adrian Mannarino katika hatua ya kufudhu kwenda kushiriki katika robo fainali ya michuano hiyo.

Djokovik ambaye yuko nafasi ya nne katika viwango vya ubora wa tennis duniani alifanikiwa kumchakaza Mannarino kwa seti 6-2 7-6 na 6-4 na kufanikiwa kutinga katika robo fainali ya michuano hiyo.

Djokovick amabye alionekana kusumbuliwa na bega katika mchezo huo sasa atakutana na mchezaji anayeahikilia nafasi ya 11 katika michuank hiyo raia wa Czech Tomas Berdych.

Mchezo huu ulipaswa kuchezwa jana lakini uliahirishwa kutoka na mchezo kati ya Rafael Nadal na Gilles Muller kuchukua muda wa masaa 4.

Na kuhusiana na bega lake Nadal amekiri kwamba bado anasikia maumivu katika bega hilo na ndio maana katika mchezo huo aliomba msaada wa madaktari mara mbili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here