Home Kimataifa Msuva,Ajib,Kichuya na wengineo, Lukaku ana ushauri huu kwenu

Msuva,Ajib,Kichuya na wengineo, Lukaku ana ushauri huu kwenu

5906
0
SHARE

Msimu uliopita wa ligi kuu ya Epl kama sio Harry Kane pengine Romelu Lukaku angekuwa mfungaji bora wa ligi hiyo, mabao 25 hayakutosha kumuondoa Kane katika kilele cha ufungaji bora.

Lukaku amekuwa mfungaji hatari tangu alipoondoka Chelsea na rekodi zinaonesha katika misimu mitano ya ligi Lukaku amefunga mabao zaidi ya 10 kwa kila msimu.

Lakini ubora wake haukuja hivi hivi bali kuna hatua alizipitia ambazo zinaweza kumfanya mchezaji yoyote kuwa bora, Lukaku alikutana na Thiery Henry na Henry alitaka kujua kuhusu mchezaji wa sasa kuwa bora.

“Ni lazima uupende mpira hilo la kwanza, mimi napenda kusoma kupitia wenzangu,naangalia sana wenzangu na napambana,hiyo ndiyo siri ya kuwa bora” alianza kuelezea Lukau jinsi ya kuwa bora.

Lukaku amesema ukiwa na vitu hivyo (kuipenda mchezo,kujituma,na kujifunza kutoka kwa wengine) baasi kila kitu kitakunyookea na vingine vitakuja vyenyewe na ubora utaongezeka.

Lukaku amesema yeye alikuwa akiwatizama sana Henry,Ronaldo na Zidane na hao alichukua baadhi ya vitu kutoka kwao na kuvihamishia katika soka lake na hiyo imemfanyia urahisi yeye wa kucheka na nyavu.

Lukaku pia amefunguka kwamba safari yake kwenda Chelsea ilitakiwa kuwa mapema sana akiwa na miaka 14 lakini mama yake hakutaka acheze kwanza soka bali ilipenda mwanaye asome ndio akacheze soka, kwa sasa mshambuliaji huyo amesaini kuitumikia Manchester United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here