Home Kimataifa Rafael Nadal “OUT” Wimbledon 2017

Rafael Nadal “OUT” Wimbledon 2017

1448
0
SHARE

Moja kati ya wacheza tennis waliotarajiwa kufanya vizuri na kubeba kombe la Wimbledon msimu huu ni Mhisapnia Rafael Nadal ambaye yuko katika ubora mkubwa katika mashindano hayo.

Lakini tofauti na matarajio ya wengi matumaini ya wengi matumaini hayo ya Nadal yamezimwa baada ya kutolewa katika mashindano hayo na raia wa Luxenbourg Gilles Muller.

Kama Nadal angeshinda mashindano haya safari hii ingekuwa ni mara yake ya tatu kushinda Wimblendon lakini Gilles aliyeko namba 16 katika viwango vya ubora wa tennis duniani amekatisha ndoto za Nadal.

Nadal alionekana kumshika Gilles katika seti mbili za mwanzo lakini baadae hali ilibadilika kwa Gilles kuukamata mchezo huo na kuisha kwa ushindi wa seti 6-3 6-4 4-6 4-6 15-13 huku mchezo huo ukitumia masaa 4 na dakika 47.

Muller amekiri kwamba mchezo huu ulikuwa mgumu sana kwake kuliko iliyopita na sasa anakwenda kukutana na Mcrotia Marin Cilic katika robo fainali ya mashindano hiyo, hii itakuwa mara ya 2 kwa Gilles kutinga katika robo fainali ya michuano mikubwa tangu alipofanya hivyo mwaka 2008 katika US Open.

Nadala ambaye ameshabeba Wimbledon mwaka 2008 na 2010 alishatabiriwa  na Roger Federer ambaye walishakutana katika fainali ya Australia Open kwamba anaweza kushinda mashindano haha ya Wembley mwaka huu,utabiri ambao unaonekana kuzimwa rasmi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here