Home Kimataifa “Ninatamani kucheza uwanja wa taifa Tanzania na kufika nchi hiyo” Wayne Rooney

“Ninatamani kucheza uwanja wa taifa Tanzania na kufika nchi hiyo” Wayne Rooney

4024
0
SHARE

Tunahesabu siku mbili tu yaani Jumanne na Jumatano lakini ikifika Alhamisi kila mtu atalekea uwanja wa taifa kushuhudia klabu ya Everton ikicheza dhidi ya Gormahia ikiwa ni sehemu ya ziara za Everton kujiandaa na msimu ujao wa ligi.

Watu walianza kukosa raha baada ya kufahamu ya kwamba Romelu Lukaku hatakuja Bongo lakini furaha kubwa imerudi kwao tena baada ya Wayne Rooney kusaini Everton na hivyo kuwepo uwezekano wa yeye kukanyaga ardhi ya Tanzania.

Yote tisa lakini kumi ni kwamba Rooney mwenyewe kwa kinywa chake ametamka kwamba anatamani sana kupajua Bongo sio tu kwa kuwajua wachezaji wenzake lakini pia kwa kuwa ni sehemu ambayo hajawahi kufika na sasa bahati imemjia anatua Bongo.

“Itakuwa safari nzuri sana, naamini na itakuwa vyema nikipata nafasi kuingia uwanjani (Wa Taifa) na kupata muda wa kucheza, sijawahi kufika Tanzania na hii itakuwa mara yangu ya kwanza lakini nina furaha kubwa kusafiri na timu” alisema Rooney.

Hii itakuwa fursa kwa Wayne Rooney na wenzake kufurahia uzuri wa nchi yetu kama walivyofanya kina Mamadou Sakho,Victor Wanyama na David Beckham ambao wote hao katika siku za karibuni walikuja Tanzania.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here