Home Kitaifa Ndemla arejeshwa Stars kuimaliza Amavubi

Ndemla arejeshwa Stars kuimaliza Amavubi

4591
0
SHARE
Said Ndemla (kulia) akishangilia goli lake na Haji Ugando (kushoto) wakati wa mechi dhidi ya Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Na Zainabu Rajabu.

KIUNGO wa Simba Said Ndemla amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachopaa jioni ya leo kwenda jijini Mwanza.

Stars inatarajiwa kupambana na timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ Julai 15 kwenye uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa michuano ya CHAN mwakani.

Ndemla aliachwa katika safari ya Afrika kusini kwenye michuano ya COSAFA kutokana na majeruhi na sasa amerejeshwa baada ya kuwa ‘fit’ tayari kulitumika taifa.

Said Ndemla Wachezaji wengine walioongezwa kikosini ni
kipa Ramadhan Kabwili (Serengeti
Boys), Boniface Maganga (Mbao FC),
Joseph Mahundi (Azam FC), Athanas
Mdamu (Alliance Academy), John Bocco
(Simba) na Kelvin Sabato (Majimaji).

Walioachwa kutokana na majeruhi ni kipa Benno Kakolanya (Yanga), Shaban Idd na Mbaraka Yusuf.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here