Home Kitaifa Timu zilizofuzu hatua ya 16 bora Ndondo Cup 2017 hizi hapa…

Timu zilizofuzu hatua ya 16 bora Ndondo Cup 2017 hizi hapa…

3174
0
SHARE

Hatimaye hatua ya makundi ya Ndondo Cup 2017 imemalizika leo baada ya mechi mbili za Kundi B kumalizika na kukamilisha jumla ya timu 16 ambazo zimefuzu kucheza hatua ya 16 bora baada ya kumaliza zikiwa na pointi nyingi kutoka kwenye makundi yao.

Mechi za Kundi B zilizokamilisha hatua ya makundi leo zilikuwa ni kati ya Kibada One vs Twiga Investment mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Air Wing huku mchezo mwingine ukipigwa kwenye uwanja wa Tandika Mabatini kati ya Burudani FC dhidi ya Madiba FC. Katika mechi hiyo, Burudani wameshinda kwa bao 4-0 na kukata tiketi ya kucheza hatua ya 16 bora baada ya kufikisha pointi saba.

Burudani FC na Kibada One zote zimemaliza zikiwa na pointi saba lakini Burudani wanaongoza kundi kundi hilo kutokana na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Msimamo wa Kundi B na timu mbili za juu zenye pointi nyingi ambazo zimefuzu kucheza hatua ya 16 bora ni kama zinavyoonekana hapa chini.

Timu 16 ambazo zimefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya Ndondo Cup 2017 kutoka Kundi A hadi Kundi H zinaonekana hapa chini huku kila kundi zikiwa zimefuzu timu mbili.

Leo usiku kupitia Sports Extra na Sports Bar, itachezeshwa droo ili kujua ni timu zipi zitapambana katia hatua ya 16 bora. Usikose kusikiliza Sports Extra ndani ya Clouds FM na kuangalia Sports Bar ya Clouds TV ili ujue timu yako itakutana na nani hatua ya 16 bora.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here