Home Kimataifa Everton Vs Gor Mahia unaweka mzigo upande upi?, Mskilize Leon Osman.

Everton Vs Gor Mahia unaweka mzigo upande upi?, Mskilize Leon Osman.

3800
0
SHARE

 

Kueleka mchezo dhidi ya mabingwa wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia, Nguli na balozi wa klabu ya Everton, Leon Osman ametamba kuwa klabu yake hiyo itaweza kuibuka na ushindi kwenye katika mchezo huo utakaopigwa dimba la taifa siku ya Julai 13.

Osman aliyasema hayo baada ya kuwasilini nchini hapo jana kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii zikiwa ni siku chache kabla ya kikosi kizima cha Everton kutua nchini.

Akiongea na SportPesa News katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye hoteli ya Sea cliff jioni ya jana, Leon alisema Everton wanajiandaa vyema kueleka mchezo huo.

“Nafikiri hivyo, kwani Everton wamekuwa wakijifua kwa wiki nzima sasa, nategemea Everton watakuja hapa na kushinda”, alitamba Leon Osman.

Hata hivyo Leon alisema anatazamia kuwa mechi hiyo dhidi ya Gor Mahia itakuwa na ushindani mkubwa kwani Gor Mahia ni timu nzuri pia.

“Bila shaka mechi hiyo itakuwa na mvuto kuitazama kwasababu Gor Mahia wamefanya kazi nzuri kwa kutwaa ubingwa wa SportPesa Super Cup ili waweze kucheza mechi na Everton. Ni fursa nzuri lakini bado nina imani kuwa Everton watashinda mechi”, alihitimisha Osman ambaye ameichezea Everton michezo zaidi ya 400 kabla ya kustaafu soka rasmi mwaka jana.

Tayari homa ya mpambano huo miongoni mwa mashabiki nchini imeendelea kuwa kubwa huku wengi wakiwa na shauku ya kuwaonya nyota mbalimbali wa Everton kama vile Jordan Pickford, Ross Barkley, Idrissa Gana Gueye na wengine wengi.

Viingilio vya mchezo huo ni Sh 8000/= kwa VIP C na Sh 3000/= kwa viti vya mzunguko na mchezo unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 jioni.

 

 

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here