Home Kitaifa Picha6: Waziri Mwakyembe alivyoipokea Stars saa 9 usiku

Picha6: Waziri Mwakyembe alivyoipokea Stars saa 9 usiku

6023
0
SHARE

Alfajiri ya leo Julai 9, 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe aliipokea timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ilipowasili Dar es Salaam ikitokea Afrika Kusini ilipokua ikishiriki michuano ya COSAFA 2017.

Mwakyembe aliungana na Makamu wa Rais wa TTFF Wallace Karia kuipoke Stars majira ya saa 9 usiku.

Stars imemaliza katika bafasi ya tatu katika micguano hiyo baada ya kuifunga Lesotho kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia mechi yao ya mshindi wa tatu kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Michuano hiyo imemsaidia kocha wa Stars Salum Mayanga kuelekea mechi za kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) ambapo Tanzania itacheza na Rwanda Julai 15, 2017.

Wachezaji wanne wa Stars walifanikiwa kuchukua tuzo ya Man of the Match (MoM) katika mechi nne tofauti. Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Elias Maguri na Erasto Nyoni ni wachezaji walishinda tuzo hiyo baada ya kufanya vyema kuisaidia Stars kupata matokeo kwenye mechi zake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here