Home Kitaifa Majina Ya Wagombea Wa Urais Wa TFF Na Nafasi Zingine Hadharani

Majina Ya Wagombea Wa Urais Wa TFF Na Nafasi Zingine Hadharani

4267
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu.

WAGOMBEA sita wamepitishwa kugombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu katika hatua za awali.

Akizungumza na Shaffidauda.co.tz Mwenyekiti wa Kamati ya  Uchaguzi, msomi Wakili Revocatus Kuuli alitaja wagombea hao kuwa ni Shija Richard, Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayai  na Emmanuel Kimbe.

“Kikao kimekaa leo na kimepitisha majina ya wagombea kwa hatua ya awali na majina yote yatabandikwa kwenye mbao za matangazo kuanzia kesho ,” alisema Wakili Kuuli.

Awali wagombea kumi walichukua fomu kuwania nafasi ya urais lakini mapema Athuman Nyamlani alijitoa hivyo majina ambayo hayakupitishwa ni Fredrick Masolwa, Jamal Malinzi na John Kijumbe kwa sababu mbalimbali.

Katika nafasi ya Makamu wa rais waliopitishwa ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Stephen Mwakibolwa na Robert Selasela huku Geofrey Nyange akielezwa kujitoa.

Katika nafasi ya wagombea wa nafasi ya kamati ya Utendaji Kocha mwenye maneno mengi Jamhuri Kihwelo, Bakari Malima, Abdallah Mussa, kwa kushindwa kuwasilisha cheti cha kuthibitisha elimu ya sekondari kwa mujibu wa kanuni ya 9(2) za uchaguzi.

Wagombea ambao hawakupitishwa kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa kanuni ya 9(3) ni Musa Sima, Salehe Alawi, Thabith Kandoro na Hassan Othuman hajapitishwa kwa kukosa uadilifu kwa mujibu wa kanuni ya 9(7) za uchaguzi wa TFF.

Zoezi la kuchukua fomu lilianza Juni 16, 2017 hadi Juni 20, mwaka huu na jumla ya wagombea 74 walichukua na kurudisha fomu kuomba kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.

Awali mchujo ulianza Juni 23, kwa mujibu wa kanuni ya 11.1 ya Uchaguzi wa TFF lakini kulitokea kutokuelewana kati ya mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Kuuli na wajumbe wa kamati hiyo hali iliyofanya Kuuli kujiuzulu kabla ya Kamati ya Utendaji ya TFF kukaa na kuivunja kamati hiyo na yeye kurejeshwa tena peke yake.

Displaying IMG-20170708-WA0097.jpg

Displaying IMG-20170708-WA0099.jpgDisplaying IMG-20170708-WA0091.jpgDisplaying IMG-20170708-WA0090.jpgDisplaying IMG-20170708-WA0092.jpgDisplaying IMG-20170708-WA0100.jpg

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here