Home Dauda TV Exclusive: Kaseja ametoa maoni na ushauri baada ya Ajib kuhamia Yanga

Exclusive: Kaseja ametoa maoni na ushauri baada ya Ajib kuhamia Yanga

23025
0
SHARE

Julai 5, 2017 klabu ya Yanga ilimtambulisha rasmi Ibrahim Ajib baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea kwa watani wao wa jadi Simba SC, uhamisho wa wachezaji kutoka vilabu hivi vikongwe nchini huwa na changamoto zake kwa wachezaji pindi wanapokutana na timu zao za zamani (Simba vs Yanga).

Dauda TV imemtafuta Juma Kaseja ambaye kwa sasa anacheza Kagera Sugar lakini amewahi kucheza katika vilabu vya Simba na Yanga kwa nyakati tofauti lengo la kumtafuta likiwa ni kutaka kupata uzoefu wake akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliovitumikia vilabu hivi vye upinzani mkubwa ndani na nje ya uwanja.

Lakini pia Dauda TV ilimuuliza Kaseja, endapo atapata fursa ya kumshauri Ajib atamwambia nini?

Dauda TV ikazungumza pia na Johans Mkarwani Mwenyekiti wa tawi la Waadilifu ambaona wanachama wa Simba ambae ametoa maoni yake kuhusu kuhusu kuondoka kwa Ajib na tetesi za Niyonzima kutua Simba.

Yote hayo utayapata kwenye video hapa chini

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here