Home Kimataifa Neymar atajwa kuwa mwanamichezo tajiri zaidi chini ya miaka 25

Neymar atajwa kuwa mwanamichezo tajiri zaidi chini ya miaka 25

5743
0
SHARE

Mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona  Neymar anetajwa na jarida la Forbes kuwa mchezaji anayeingiza fedha nyingi zaidi kwa wanamichezo waliochini ya umri wa miaka 25. 
Neymar, ambaye atatimiza miaka 26 February 2018, ameingiza kiasi cha $37m, mbele ya mcheza golf Jordan Spieth ($34.5m) na wachezaji  wa NBA Kyrie Irving ($29.9m) na Anthony Davis ($28.1m).

Mbrazil huyo alisaini mkataba mpya wa kiaka 5 na Barcelona ambao una thamani ya $15m kwa mwaka, lakini pia Neymar anaripotiwa kuingiza fedha nyingi zaidi kutokana na mapato ya matangazo ya biashara. 

Neymar ndio mwanasoka pekee ambaye anaingiza fedha nyingi zaidi nje ya uwanja kuliko anazopata kutokana na soka moja kwa moja kupitia mikataba yake na Nike, Gillette, Panasonic na Beats by Dre. 

Katika listi ya wanamichezo walioingiza fedha nyungi zaidi kwa ujumla – Neymar anashika nafasi ya 18 kati ya wana michezo 100.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here