Home Kitaifa Mabosi Simba watua Keko kuwaona Aveva, Kaburu.

Mabosi Simba watua Keko kuwaona Aveva, Kaburu.

4878
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu.

BAADHI ya viongozi wa Simba, leo Jumapili waliwatembelea katika Gereza la Keko, rais wa klabu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu

Aveva na Kaburu wapo gerezani hapo baada ya kufikishwa Alhamisi iliyopita wakituhumiwa kwa makosa matano ikiwemo la utakatishaji fedha.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ndiyo wamewashitaki viongozi hao ambapo baada ya kusomewa mashitaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Alhamisi iliyopita, walinyimwa dhamana na kupelekwa mahabusu ambapo kesi hiyo itatajwa tena Julai 13, mwaka huu.

Viongozi ambao walifika leo asubuhi kuwaona Aveva na Kaburu, ni Said Tully, Musleh Al Rawah, Haji Manara na Ally Suru.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here