Home Kimataifa Bradley Lowery amuaga Defoe huku akihema kwa tabu

Bradley Lowery amuaga Defoe huku akihema kwa tabu

6320
0
SHARE

Wakati Jermain Defoe anajiandaa kuhamia kabisa na familia yake katika klabu ya Afc Bournamouth ameamua kuwaaga watu wake wote wa karibu waliokuwa wakimoa support wakati akiwa na klabu ya Sunderland.

Kijana anayesumbuliwa na maradhi ya kansa Bradley Lowery anafahamika kama mtu aliyekuwa karibu na Defoe na kumpa support kubwa sana akiwa Sunderland pamoja na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.

Bradley ameona Defoe asiondoke hivi hivi na kuamua kumualika ngumbani kwao ili kumuaga, katika party hiyo Bradley ambaye bado anaumwa alimualika pia mpenzi wake aitwaye Poppy ili kumuaga kwa pamoja mshambuliaji huyo.

Taarifa za kusikitisha zinasema Bradley pamoja na party hiyo lakini alikuwa akiitafuta pumzi kwani alikuwa akihema kwa tabu sana huku binamu zake pamoja na mchezaji huyo kumkumbatia hadi akasinzia.

Katika taarifa iliyoandikwa na familia yake ilisema “amekuwa hoi sana kwani hata pumzi amekuwa akiipata kwa tabu sana na kupumua kwake kumebadilika ila aliomba kufanya party ya kukutana na watu wake wa karibu na wote awapendao”

Mama wa mtoto huyo amekiri kwamba hali ya Bradley siyo nzuri hata kidogo lakini akasisitiza kwamba kijana wake huyo anaendelea kupambana kuibakisha pumzi yake na kumshukuru Defoe kwa kuwa mtu muhimu sana kwa kijana wake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here