Home Kimataifa Arsenal wakaribia kuua ndege wawili kwa jiwe moja, Lacazatte na Sanchez

Arsenal wakaribia kuua ndege wawili kwa jiwe moja, Lacazatte na Sanchez

5876
0
SHARE

Inafahamika nchini Ufaransa ya kwamba uhamisho wa Alexandre Lacazette kwenda Arsenal kwa dau la €50 unakaribia sana kutokea katika wiki inayokuja.

Taarifa kutoka Ufaransa zinadai baadhi ya maofisa wa klabu ya Arsenal walisafiri hadi nchini Ufaransa kwenda kukutana na wakala wa Lacazette kukamilisha dili hilo.

Pamoja na raisi wa klabu ya Lyon kusema kwba Lacazette hawezi kwenda Uingereza msimu huu lakini taarifa zinadai dau lililotumwa na Arsenal limewashawishi Lyon kumuuza Lacazzete.

Wakati Lacazatte akijiandaa kwenda Arsenal kama inavyosemwa, ripoti zingine zinadai klabu hiyo imefanikiwa kumbakisha Alexis Sanchez katika kikosi hicho.

Hadi sasa hakuna ofa yoyote rasmi iliyoletwa mezani kwa ajili ya kumnunua Sanchez suala linalomaanisha kwamba klabu hiyo inaweza kuishinda vita ya kumbakisha klabuni hapo Sanchez.

Endapo Sanchez atabaki Arsenal na Lacazette atakwenda katika klabu hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kutengenezwa kwa pacha kali ya ushambuliaji katika klabu hiyo msimu ujao wa ligi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here