Home Kitaifa Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mwesigwa wamenyimwa dhamana

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mwesigwa wamenyimwa dhamana

3713
0
SHARE

Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa na Afisa wa fedha wa TFF Nsiande Mwanga wote kwa pamoja wamesomewa mashitaka ya jinai katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wanakabiliwa na mashitaka 28, katika mashitaka hayo Jamal Malinzi anakabiliwa na mashitaka zaidi ya 25 mengi yakiwa ni ya kughushi nyaraka katika michakato ya malipo mbalimbali.

Imeelezwa kwamba, kuna wakati Malinzi alikua anaandika risiti za kujilipa akidai kwamba aliikopesha TFF.

Lakini katika makosa hayo 28 kuna makosa matatu ya utakatishaji fedha yanawakabili, kuna kosa moja la utakatishaji fedha linalowakabili wote kwa pamoja. Kuna shitaka jingine linawakabili Malinzi na Mwesigwa huku kosa moja likimkabili Bi. Mwanga pekeake.

Watuhumiwa wote wamekana mashitaka yanayo wakabili imeahirishwa hadi July 3, 2017 ambapo kutatolewa uamuzi kuhusu dhamana kwa watuhumiwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here