Home Kimataifa Barua ya wazi ya Alves kwenda Juve, asisitiza hachezi kwa ajili ya...

Barua ya wazi ya Alves kwenda Juve, asisitiza hachezi kwa ajili ya pesa

5801
0
SHARE

Tayari klabu ya Juventus imethibitisha kwamba hawatakuwa na Dani Alves katika msimu ujao wa ligi baada ya mlinzi huyo kuamua kutorndelea kukukipiga katika klabu hiyo ya Italia.

Tayari timu mbalimbali zimesanza kuwinda saini ya Alaves lakini Manchester City wanaonekana wako karibu zaidi kumsajili mlinzi huyo wa kimataifa wa Brazil.

Baada ya Alves kusema kwamba hataendelea Juventus, mashabiki wengi walimshambulia kuwa na tamaa ya pesa, na sasa Alves ameibuka na kuandika ujumbe wa majonzi kuiaga Juventus.

“Nawashukuru sana mashabiki wa Juventus walioishi na mimi mwaka mzima na kunipa support kama mchezaji wao katika timu hii inayochukua makombe na kucheza fainali” alianza kuandika Alves.

“Kwa heshima ya klabu hii nilijitoa sana na kupambana sana ili kuifanya klabu hii kuwa klabu kubwa zaidi ulimwenguni na hii ilitokana na kupafurahia hapa”

“Naomba msamaha sana mashabiki wa Juventus kwa kama kuna siku niliwakosea lakini sikuwahi kukusudia kufanya hivyo, hakuna mwanadamu aliyeko sawa lakini lakini sikuwahi kukusudia kuwaudhi”

“Sichezi mpira kwa sababu ya pesa kama inavyodaiwa bali nacheza mpira kwa sababu naupenda mpira na watu wake,nawaachia ninyi munihukumu kwa kazi niliyowatendea” alimalizia Alves.

Alves pia alimshukuru CEO wa Juventus Beppe Marrota ambaye ndiye ametoa ruhusa kwa Alves kuondoka katika klabu hiyo mabingwa wa Serie A.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here