Home Kitaifa Tetesi: Niyonzima apewa jezi ya Kazimoto Simba.

Tetesi: Niyonzima apewa jezi ya Kazimoto Simba.

15966
0
SHARE

Baada ya timu ya Simba kukamilisha usajili wa kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima usajili ambao ulikuwa unaogelewa sana na wapenzi wa Soka hapa nchi, taarifa mpya ni kwamba kiungo huyo atapewa jezi namba 8.

Kiungo huyo machachari ameacha na Yanga baada ya kucheza misimu sita mfululizo na amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya zaidi ya  milioni 100 za Kitanzania.

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, Haruna atapewa jezi hiyo iliyokuwa ikitumiwa na Mwinyi Kazimoto.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kazimoto hayupo kwenye mipango ya mwalimu kwa msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika.

Haruna ambae ni kipenzi cha wana Yanga, atatumbulishwa rasmi na timu yake mpya katika sherehe za Simba Day Agosti, mwaka huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here