Home Kitaifa Peter Manyika kuhusu viongozi kusajili wachezaji badala ya makocha

Peter Manyika kuhusu viongozi kusajili wachezaji badala ya makocha

8254
0
SHARE

Ikiwa ni kipindi cha dirisha la usajili, ambapo timu mbalimbali zikiimarisha vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara huku timu nyikine zikifanya usajili kwa ajili ya michuano ya kimataifa, Peter Manyika golikipa wa zamani ametoa maoni yake kuhusu usajili unaofanywa.

Manyika amesema bado anagubikwa na utata kwa namna usajili unavyofanyika hapa nyumbani huku viongozi ndio wakisajili wachezaji, baba huyo wa golikpa wa Simba Manyika Jr amesema si tatizo viongozi kusajili wachezaji lakini akahoji, wachezaji wanaosajiliwa ni wale wanaohitajiwa na kocha?

“Sasa hivi viongozi wanajibebesha madaraka makubwa kutokana na vyeti, zamani timu zilikuwa zinaongozwa na wazee ambao hawana vyeti na timu zilikuwa zinacheza kwa mafanikio lakini sasa hivi viongozi wengi wa timu wapo kwenye timu kwa ajili ya maslahi yao.”

“Usajili unaofanyika utacheka, hata mimi nashindwa kuelewa. Inakuwaje unamchukua mchezaji wa kiwango cha chini na kumwacha wa kiwango cha juu hii haiingii akilini dunia nzima.”

“Hata mimi ukinipa klabu kuiongoza katika usajili, nitakufanyia usajili mzuri sana kuliko kiongozi mwenye pesa kwa sababu nitaangalia vigezo vinavyotakiwa. Mpira ni mchezo wa hadharani, inakuwaje mtu anaiua timu badala ya kuirekebisha, sasa sijui wanasajili kimaslahi au kiundugu, sijaelewa vizuri hapo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here