Home Kitaifa ‘Nimejiandaa vizuri kuachana na Azam’ – Manula

‘Nimejiandaa vizuri kuachana na Azam’ – Manula

10728
0
SHARE

Golikipa wa Azam FC Aishi Manula amesema ameshajiandaa kiakili kuachana na klabu yake ya sasa na kwenda katika klabu yake mpya mara baada ya mkataba wake kumalizika.

“Kumekuwa na maswali mengi kwamba kwa nini umekwenda Simba kwa sababu wanaamini hivi vilabu vikubwa vinaharibu viwango vya wachezaji na wachezaji wengi ambao wameenda huko huwa wanapatwa na mataizo hasa ya mikataba na kutopewa mishahara.”

“Niwahakikishie, mimi nakwenda kujiunga na moja ya hivyo vilabu nikiwa najua hayo yote. Kiujumla nimejiandaa na hayo yote yatakayotokea nimeshajiandaa nayo kwa hiyo nakwenda sehemu ambayo najua tayari kwamba kuna matatizo ya kucheleweshewa mishahara.”

“Watu wa nje ambao hawajui wanaamini Azam kuna maisha mazuri na hawajui hali halisi ambayo ipo ndani ya Azam, wote tulikuwa Azam na maisha ya pale tunayajua. Mimi siyo mpumbavu wa kiasi hicho kuondoka Azam huku nikiwa najua sehemu ambayo kilakitu kipopo halafu naenda sehemu ambayo vitu hivyo havipo.”

“Wanatakiwa waelewe mimi kama mchezaji kuna vitu ambavyo natakiwa niwe navyo kwa sababu ninafamilia na inahitaji huduma kutoka kwangu, siwezi kuwa na familia halafu haipati huduma wanayostahili au ambayo wanadhani wanastahili pale nilipokuwa.”

“Napenda kuwaambia viongozi wangu wa Azam kwamba, kama walivyopanga kupandisha vijana hiki ni kitu kizuri kwa sababu hata mimi nilipata nafasi baada ya kupandishwa kutoka timu ya vijana na wengi wetu tukafanya vizuri.”

“Nilisikia kiongozi mmoja mmoja akiongea kwa hisia juu yangu kwamba wamenilea na kunifundisha vitu vingi ndani na nje ya uwanja lakini naondoka kirahisi, lakini hata mimi naondoka Azam huku nikiwa bado naipenda sio kwamba nafurahia kuondoka Azam kwa sababu nakumbuka vitu ambavyo wamenifanyia lakini naondoka kwa sababu.”

“Tunaona Leonel Messi ametoka kwenye academy ya Barcelona na bado yupo hadi leo na ukiangalia ndio mchezaji anaelipwa pesa nyingi kuliko mtu mwingine yeyote lakini kulelewa tu bado haitoshi kuweza kupata kiasi kile ambacho wao wanadhani nastahili kupewa kiasi walichotaka kunipa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here