Home Kimataifa Picha: Mzamiru Yassin ametisha, Stars inaongoza Kundi COSAFA

Picha: Mzamiru Yassin ametisha, Stars inaongoza Kundi COSAFA

23046
0
SHARE

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetoka sare ya 0-0 dhidi ya Angola kwenye mechi ya Kundi A michuano ya COSAFA mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Royal Bafokeng, Rustenburg, Afrika Kusini.

Matokeo hayo ya sare yanaendelea kuifanya Stars iongoze kundi lake kutokana na wastani mzuri wa magoli huku ikiwa inalingana pointi na Angola (timu zaote zina pointi nne) baada ya kila timu kucheza mechi mbili.

Kiungo wa Tanzania Mzamiru Yassin ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo ‘Man of the Match’ baada kuonesha kiwango cha juu wakati wote wa mchezo huo.

Ni mara ya pili mfululizo tuzo ya Man of the Match inachukuliwa na mchezaji wa kitanzania, mechi ya kwanza Shiza Kichuya alitangazwa mchezaji bora wa mechi kufuatia kuifungia Stars magoli mawili yaliyoipa ushindi dhidi ya Malawi.

Aishi Manula alifanya kazi ya ziada kupachi mpira wa kona dakika ya sita tu tangu kuanza kwa mchezo wakati Angola walipokuwa wakitafuta goli la dakika za mapema.

Angola walilazimika kufanya mabadiliko dakika ya 23 kipindi cha kwanza kufuatia Natael kupata majeraha na nafasi ya ikachukuliwa na beki mwenzake Carneiro.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here