Home Kimataifa “Mtamkumbuka na Mtalia” Lampard awaambia Chelsea kuhusu Costa

“Mtamkumbuka na Mtalia” Lampard awaambia Chelsea kuhusu Costa

5911
0
SHARE

Tayari kocha Antonio Conte amemuambia Diego Costa atafute pakucheza msimu ujao, hilo linakuja baada ya mshambuliaji huyo kutoa mchango mkubwa sana kwa klabu ya Chelsea na kuifanya kuchukua ubingwa EPL.

Sasa kiungo wa zamani wa Chelsea Frank Lampard amewaonya Chelsea kuhusu Costa na kusisitiza kwamba itawachukua muda na itakuwa ngumu sana kwao kumtafuta Diego Costa mwingine.

Lampard anaona duniani kwa sasa kuna uhaba wa washambuliaji aina ya Diego Costa na timu nyingi zinatamani kuwa na mchezaji wa namna yake, hivyo Chelsea itawagharimu sana kumuacha aondoke.

“Hata sielewi, haihitaji kuongea sana kuhusu yeye kwani kila kitu kinaonekana wazi, tangu amekuja Chelsea amekuwa akionesha kiwango cha hali ya juu sana na nina mashaka makubwa kama wataweza kuziba pengo lake” alisema Lampard.

Tangu ajiunge na klabu ya Chelsea mwaka 2014 mshambuliaji huyo wakimataifa toka nchini Hispania amekuwa akiongoza kwa ufungaji katika klabu hiyo kwa misimu mitatu mfululizo na akiwasaidia kubeba makombe.

Lampard anasema Lukaku kweli ni mzuri sana lakini ununuzi wake ni ghali na anaona ni bora wabaki na Costa ambaye ana kila kitu ambacho mshambuliaji yoyote duniani anapaswa kuwa nacho.

Baada ya Antonio Conte kumtosa Diego Costa tayari baadhi ya vilabu vimeshaanza kutafuta saini yake lakini mwenyewe Diego Costa anatamani kurudi mahali Chelsea walipomtoa ambapo ni Atletico Madrid.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here