Home Kitaifa Matokeo ya mechi za Ndondo Cup leo Juni 27, 2017

Matokeo ya mechi za Ndondo Cup leo Juni 27, 2017

4858
0
SHARE

Misosi FC imekuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup 2017 baada ya kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Mdandu Investment mechi iliyopigwa uwanja wa Kinesi pale V. Wanyama Street, Shekilango.

Laurent Mugila aliifungia Misosi bao la kwanza dakika ya 17 kipindi cha kwanza kabla ya Fuluzuri kufunga goli la pili dakika ya 40 na matokeo kuwa Misosi 2-0 Mdandu hadi mapumziko.

Maganga akapasia kamba tena dakika ya 63 kipindi cha pili likiwa ni bao la tatu na la ushindi kwa Misosi ambao wanaongoza kundi lao wakiwa na pointi sita baada kushinda mechi zao mbili za kwanza mfululizo huku wakiwa wamebakiza mechi moja ya hatua ya makundi.

Kwenye uwanja wa Mwl. Nyerere, Magomeni, Buguruni wamepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Kibo Kombaini.

Goli pekee katika mchezo huo limefungwa na Twaha Magoha dakika ya 30 kipindi cha kwanza na kudumu hadi dakika ya 90 ya mchezo huo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here