Home Kitaifa Boban ataka kurejea Simba

Boban ataka kurejea Simba

8271
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu.

MCHEZAJI wa zamani wa Simba, Haruna Moshi Boban anatamani kurudi katika timu yake ya zamani ya Simba.

Haruna aliwahi kucheza Simba akiwa  na Emmanuel Okwi na Shomary Kapombe kwa mafanikio makubwa na kupata bahati ya kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania kabla ya kurejea nchi ambapo kwa sasa hana timu ya kuichezea katika ligi kuu.

Akizungumza na Shaffidauda.co.tz. mara baada ya mchezo wa michuano ya Sports Extra Ndondo Cup akiitumikia Faru Jeuri iliyocheza na FC Kauzu,  Boban alisema anatamani siku moja arudi kuichezea Simba kama watamuhitaji.

“Simba imefanya vizuri kuwarejesha kundini wachezaji Emmanuel Okwi na Shomary Kapombe ni wachezaji wazuri na watawasaidia sana katika msimu ujao”alisema Boban.

Boban jana aliisaidia timu yake ya Faru Jeuri kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Kauzu mchezo uliofanyika Katika Dimba la Kinesi na kuhudhuriwa na mchezaji wa Tottenham Hotspur , Mkenya Victor Wanyama ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here