Home Kitaifa Safari ya Victor Wanyama kutoka Kenya hadi Tottenham

Safari ya Victor Wanyama kutoka Kenya hadi Tottenham

5381
0
SHARE

Victor Wanyama ameelezea safari yake ya soka tangu alivyoondoka Afrika kwenda Ulaya na baadae kufanikiwa hadi kucheza Tottenham sehemu ambayo anaamini anaweza kutimiza ndoto yake ya kutwaa vikombe kwa sababu yupo kwenye moja ya timu zenye ushindani Duniani.

Wanyama aliondoka Kenya kwenda Ulaya akiwa bado mdogo tofauti na wengi wanavyofahamu na alikwenda huko kutembea lakini alipopata fursa akaonesha kipaji chake na hapo ndipo safari rasmi ya soka lake barani Ulaya ikaanza.

“Mimi nilienda nje nikiwa bado mdogo, nilianzia Sweden halafu nikaenda Ubelgiji ambako nilikaa sana kama miaka mitano halafu nikachukuliwa na Celtic lakini ilikuwa ngumu kupata kibali cha kufanyia kazi ilikuwa ni ngumu kwa sababu rank za Kenya hazikuwa poa zilikuwa hazijavuka kiwango kinachotakiwa lakini nilikuwa nina miaka 18 kwa hiyo nikapata bahati ya kuchukuliwa kama special talent nikafanikiwa kuingia.”

“Ndugu yangu Mariga alikuwa Sweden kwa hiyo mimi nilienda kama kutembea kufika kule akaenda kuuliza kwenye klabu yake kama naweza kufanya mazoezi, wakakubali niende nikafanye nao mazoezi nikaenda wakanipenda wakataka niendelee kuwa nao.”

“Mariga akapata deal Italy kwenye klabu ya Parma nikamuomba twende pamoja akakataa akaniambia lazima kila mtu awe na njia yake na hapo ndio nitakomaa kimpira, nikakubaliana nae.”

“Tukapata tournament huko Sweden tukacheza na timu kutoka Ubelgiji na kulikuwa na scout kutoka Kenya akaniona hapo halafu akaniambia nirudi Kenya, nikarudi nikafanya nao mazoezi kwa miezi mitatu akanipeleka Ubelgiji.”

“Spurs nimefika na kuna vitu inabidi nivikamilishe, ndoto yangu imekuwa ni kushinda vikombe na kwa sasa nimepata klabu ambayo naweza kutimiza nayo malengo yangu ya kushinda vikombe halafu badae tutaona.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here