Home Dauda TV Video: Msuva amezungumza kuhusu Niyonzima kuondoka, kuvunja mkataba na tetesi za Ajib...

Video: Msuva amezungumza kuhusu Niyonzima kuondoka, kuvunja mkataba na tetesi za Ajib kusaini mkataba Yanga

32475
0
SHARE

Dauda TV imepiga story na star wa Yanga na Taifa Stars Simon Msuva ambaye amezungumzia mambo kadhaa ambayo wadau wengi wa soka wangependa kujua kutoka kwake.

Msuva ameanza kwa kueleza namna alivyostushwa na taarifa ya Yanga kushindwa kufikia mwafaka na Haruna Niyonzima na klabu hiyo kuamua kumwacha Niyonzima aende mahali pengine kuendelea na soka.

Kumekuwa na tetesi kwamba Msuva amevunja mkataba na Yanga baada ya klabu hiyo kutomlipa kwa muda, Msuva ameeleza nini kinaendelea hadi sasa, lakini pia amefafanua kuhusu ofa alizopata za kwenda kucheza nje ya Tanzania.

Inatajwa kwamba Ibrahim Ajib ameshamalizana na Yanga huku ikisubiriwa muda tu ili mshambuliaji huyo atangazwe rasmi, Msuva amesema anaamini Ajib ataisaidia Yanga kutokana na uwezo wake uwanjani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here