Home Kimataifa Wakati Everton wakijiandaa kuja bongo, tayari mchezaji wao huyu yuko Arusha na...

Wakati Everton wakijiandaa kuja bongo, tayari mchezaji wao huyu yuko Arusha na mkewe

5027
0
SHARE

Sports Pesa wameamua kukata kiu kwa mashabiki wa soka wa Epl kwa kuwaletea klabu ya Everton nchini Tanzania ambapo tutawaona live pale uwanja wa taifa.

Lakini wakati Everton wakijipanga kuja nchink Tanzania tayari kiungo wao Mfaransa ambaye mwanzo alikuwa akikipiga Manchester United Morgan Schnerdelin yuko nchini Tanzania na mkewe wanakula bata.

Morgan ameonekana akipiga picha na wamasai huku akiwa na mkewe wakiwa kaskazini mwa Tanzania ambako wamekuja kwa ajili ya mapumziko baada ya ndoa (honeymoon).

Mke wa Morgan aitwaje Camille walifunga ndoa na Morgan mwanzoni mwa mwezi huu na baadae waliamua kutafuta sehemu nzuri kwa ajili ya mapumziko na ndio wamekuja Tanzania.

Camille alikuwa ni mtangazaji na pia ni muigizaji na kati ya picha alizoweka mtandaoni aliandika maandishi yanayosema “niko hoteli nzuri sana katikati ya pori, KARIBU TANZANIA”.

Tayari ujio wa Everton ni gumzo kubwa sio tu Tanzania bali na Afrika Mashariki kwa ujumla na tayari Sports Pesa wanahakikisha kila mshabiki wa soka anaburudika na ujio huo

.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here