Home Dauda TV Video: Aishi Manula amejibu kuhusu kusajiliwa Simba na mkataba wake na Azam

Video: Aishi Manula amejibu kuhusu kusajiliwa Simba na mkataba wake na Azam

23525
0
SHARE

Golikipa wa Azam na Taifa Stars Aishi Manula amesema hajasaini mkataba na timu yoyote kama ambavyo taarifa zinavumishwa kwamba tayari amesha malizana na wekundu wa Msimbazi Simba.

Lakini Manula amesema pindi mkataba wake na Azam utakapo malizika hatoendelea kuitumikia klabu hiyo na ataondoka Chamazi na kuelekea sehemu nyingine.

Manula ameiambia Dauda TV kwamba, bado ataendelea kucheza nchini kwa msimu ujao na ataweka wazi atakuwa timu gani mara baada ya mkataba wake na Azam kumalizika.

Taarifa zinaeleza kwamba Manula akimaliza mkataba wake ndani ya Azam atatangazwa rasmi na klabu ya Simba kwani tayari wameshamalizana na mshindi huyo wa tuzo ya golikipa bora wa msimu uliopita (2016/2017).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here