Home Kimataifa Tetesi za usajili kutoka Arsenal, Manchester United, Chelsea na Liverpool

Tetesi za usajili kutoka Arsenal, Manchester United, Chelsea na Liverpool

16604
0
SHARE

Liverpool.Baada ya juhudi za muda mrefu kumsaka winga wa As Roma hatimaye taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema Mohamed Salah yuko nchini humo ili kufanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na klabu ya Liverpool.

Inasemekana toka siku ya Jumanne Salah alikuwepo Marseyside kwa ajili ya kukamilisha dili hilo ambalo litaigharimu klabu ya Liverpool kiasi cha euro 38million.

Chelsea.Wakati Liverpool wao wakikamilisha usajili wa winga huyo kutoka ligi ya Serie A, wenzao Chelsea nao wamepiga hodi katika ligi hiyo hiyo ya Serie kujaribu kutafuta mlinzi atakayeimalisha ngome yao ya ulinzi.

Taarifa zinasema raisi wa klabu ya Juventus Beppe Marotta amesema wamepokea ofa nzuri kutoka katika klabu ya Chelsea kwa mlinzi wao Alex Sandro, japokuwa hakuna taarifa rasmi kuhusu kiasi kilichotumwa na Chelsea lakini inasemekana ni zaidi ya euro 70m.

Chelsea.Katika klabu hiyo hiyo ya Chelsea inasemekana baada ya Diego Costa kutoswa na kocha wake Antonio Conte sasa mshambuliaji huyo amewaambia Chelsea kwamba anataka arudi alikotoka(Chelsea).

Manchester United.Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na klabu ya Real Socieadad kumuuza winga wao Adnan Januzaj ambaye anatarajia kujiunga na Wahispania hao kwa dau la euro 9.7m.

Manchester United.Mshauri wa mshambuliaji Cristiano Ronaldo amesema hakuna klabu Uingereza inaweza kumchukua Ronaldo zaidi ya Manchester United kwani hapo ndipo Ronaldo anapopawaza zaidi.

Arsenal.Hatimaye klabu ya Arsenal imewaweka wazi Barcelona ambao wanamtaka Hector Bellerin kwa kuwaambia kwamba wafanye tu mambo mengine kwani beki huyo hawezi kuuzwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here