Home Kitaifa Hat-trick ya nne imefungwa Ndondo Cup 2017

Hat-trick ya nne imefungwa Ndondo Cup 2017

3646
0
SHARE

Miraji Athumani amefunga magoli matatu kwenye mechi ya Ndondo Cup wakati timu yake ya Mpakani Kombaini ikiibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Vijana Rangers kwenye uwanja wa Kinesi, Sinza, Dar es Salaam.

Athumani alianza kupasia kamba dakika ya 16 na 19 kipindi cha kwanza mabao yaliyoifanya Mpakani Kombaini kwenda mapumziko ikiongoza 2-0 dhidi ya Vijana.

Kipindi cha pili dakika ya 61 Athumani akakamilisha hat-trick yake kwenye mchezo huo uliomalizika kwa Mpakani Kombaini kuondoka na pointi zote tatu.

Hat-trick hiyo ni ya nne kufungwa kwenye michuano ya Ndondo Cup 2017 tangu mashindano yalipozinduliwa rasmi Juni 17 kwa hatua ya makundi.

Baada ya mechi kumalizika, Miraji Athumani alikabidhiwa mpira wake na mwamuzi wa mchezo huo, mpira rasmi wa mashindano ya msimu huu ulitengenezwa na kampuni ya Sports Master.

Goli pekee la Vijana Rangers limefungwa na Yahaya Mbegu dakika ya 71.

Kwenye uwanja wa Mwl. Nyerere Magomeni, Tabata United wamepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Wauza Matairi na kufanikiwa kukusanya pointi tatu muhimu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here