Home Ligi EPL Fabinho: Ofa ya Man Utd itanishawishi sana

Fabinho: Ofa ya Man Utd itanishawishi sana

17686
0
SHARE

Inaonekana wachezaji wa kibrazil wamekuwa wepesi kuzungumzia matamanio yao ya kujiunga na Manchester United hadharani katika siku za hivi karibuni. 
Wiki iliyopita alikuwa Anderson Talisca, alipokuwa akiongea na Globo Esporte, alipoulizwa kuhusu kocha wa United, Jose Mourinho alisema angependa kumtumikia Jose na anaamini kuna uwezekano uhamisho wa kwenda United utawezekana.
Na jana ilikuwa zamu ya kiungo wa Monaco, Fabinho kumzungumzia Mourinho na Manchester United. Fabinho alikuwa akihojiwa na na Esporte Interativo, na alipoulizwa atasijikiaje kuhusu kuhamia Manchester United ikiwa wakileta ofa rasmi. 
Fabinho akajibu: “Litakuwa jambo lenye majaribu makubwa. Kwanza nitazungumza na wakala wangu, timu yangu Monaco, ili niweze kuamua kila kitu vizuri. United ni klabu kubwa hivyo itanibidi nifikirie vizuri kuhusiana na hilo.” 

Jana Alhamisi gazeti kubwa la nchini Italia Corriero Dello Sport liripoti kwamba United imekubaliana na Monaco kulipa kiasi cha €35m + €5m za bonasi ili kumsaini kiungo huyo wa Monaco mwenye umri wa miaka 23. 
.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here