Home Uncategorized Usajili wa Cr7,Mbappe na Mohamed Salah wachukua sura mpya.

Usajili wa Cr7,Mbappe na Mohamed Salah wachukua sura mpya.

8866
0
SHARE

Habari kuhusu Cristiano Ronaldo kuondoka Real Madrid ndio habari kubwa kwa sasa katika vyombo vingi vya habari lakini utata unakuja pale wanahabari wanaposhindwa kujua ni wapi haswa Ronaldo anakwenda.

Mlinzi wa Real Madrid Pepe ambaye msimu ujao atakuwa na uzi wa PSG amemshauri Ronaldo asiende Manchester United bali aende PSG ili wakacheze tena pamoja kama ilivyo wakiwa Real Madrid na Ureno.

Lakini gazeti maarufu la Marca limeibuka na kichwa cha habari kuhusu Kylian Mbappe bapo limesema nyota huyo atahamia katika klabu ya Real Madrid hivi karibuni kwa dau la euro 100m.

Marca linasema klabu ya Real Madrid pekee ndio klabu ambayo inaweza kumchukua Mbappe na na ka miamba hiyo ya Hispania ikashindwa baasi nyota huyo atabaki katika klabu yake ya sasa ya Monaco.

Kuhusu Salah na Liverpool mwishoni mwa wiki kulisambaa picha inayomuonesha shabiki akiwa amepiga picha na winga huyo na kuandika “nakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya na Liverpool’

Baada ya picha hiyo kusambaa sana wakala wa Salah aitwaye Rammy Abbas ameibuka na kusema anashanngazwa na watu wanavyoamini picha za mashabiki wakati ilikuwa ni habari ya uongo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here