Home Kitaifa Matokeo ya Ndondo Cup 2017 Mlalakuwa Ranger vs FC Goroka

Matokeo ya Ndondo Cup 2017 Mlalakuwa Ranger vs FC Goroka

2793
0
SHARE

Mechi za Ndondo Cup 2017 hatua ya makundi zimeendelea leo ikiwa ni siku ya tatu tangu mashindano ya msimu huu yalipozinduliwa rasmi Jumamosi Juni 17, 2017.

Leo Juni 19, 2017 imechezwa michezo miwili tofauti, kwenye uwanja wa Mwl. Nyerere kulikuwa na mechi kati ya Mlalakuwa Rangers dhidi ya Goroka ambapo mchezo huo umemalizika kwa Malalakuwa ikiibamiza Goroka kwa magoli 4-0.

Mapema tu Mlalakuwa walianza kupata bao dakika ya 16 kipindi cha kwanza lililofungwa na Herry Mkongo kisha Kiggy Makasy akaifungia tena Mlalakuwa bao la pili dakika 10 baadae baada ya goli la kwanza kufungwa.

Kipndi cha kwanza kikamalizika Mlalakuwa wakiwa mbele kwa magoli 2-0 na timu hizo zikaelekea mapumziko kwa ajili ya kupata maneno mawili-matatu kutoka kwenye mabenchi yao ya ufundi.

Dakika 45 za kipindi cha pili, Goroka walijitahidi kupambana kusawazisha lakini bado hawakufanikiwa na wakati dakika zikiwa zinaelekea ukingoni, Mlalakuwa wakafunga magoli mawili ya harakaharaka. Ayoub alifunga goli la tatu dakika ya 86 na Fakh Hakika akakamisha ushindi wa magoli manne kwa kuifungia Mlalakuwa bao la nne.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here