Home Kitaifa Ally Mayay kajitosa Urais TFF

Ally Mayay kajitosa Urais TFF

7517
0
SHARE

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga na Taifa Stars Ally Mayay ‘Tembele’ leo Juni 19, 2017 amechukua fomu ya kugombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF).

Mayay sambamba na mchezaji mwingine wa zamani Mtemi Ramadhani walifika TFF kwa ajili ya kuchukua fomu ambapo Mtemi Ramadhani yeye anawania nafasi ya makamu wa Rais wa TFF.

Wawili hao walisindikizwa ofisi za TFF na wadau mbalimbali wa soka wakiongozwa na kocha Jamhuri Kiwelu ‘Julio’ pamoja na wachezaji wa zamani wa soka akiwemo Jembe Ulaya.

Msafara wa Mayay ulikuwa umebeba mabango yenye ujumbe unaosomeka “Turudishieni mpira wetu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here