Home Kitaifa Polisi na Lyanga wao wamepigwa na watoto wa sokoni

Polisi na Lyanga wao wamepigwa na watoto wa sokoni

8869
0
SHARE

Maafande wa Polisi (Dar es Salaam Polisi Collage) wameshindwa kufurukuta kwa watoto wa sokoni Temeke Market baada ya kuchezea bao 1-0 kwenye mechi ya Ndondo Cup ilichezwa kwenye uwanja wa Tandika Mabatini.

Bao pekee katika mchezo huo limefungwa dakika ya 29 kipindi cha kwanza na Nassoro Kapamba na kuipa ushinda Temeke Market ambao ndio mabingwa watetezi wa taji la Ndondo.

Katika mechi hiyo, ameonekana mchezaji wa zamani wa Simba na ligi kuu Tanzania bara Daniel Lyanga ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa kwenye falme za kiarabu.

Lyanga anaitumikia timu ya Dar Police Collage katika michuano hii ya Ndondo Cup 2017.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here