Home Kimataifa Ni miaka 10 imepita tangu Foe afariki dunia,Cameroon wanarudi Confedaration Cup.

Ni miaka 10 imepita tangu Foe afariki dunia,Cameroon wanarudi Confedaration Cup.

3527
0
SHARE
SAITAMA 06/06/2002 MONDIALI 2002 CAMERUN - ARABI SAUDITA NELLA FOTO FOE marc vivien FOTO ALDO LIVERANI

Ilikuwa ni mwaka 2003 nakumbuka pale nchini Ufaransa tukiishuhudia Cameroon ikiifunga Brazil na Uturuki na kufudhu kwa hatua iliyofuata ya Confedaration Cup na Waafrika tulijawa na furaha kutokana na Cameroon ile ya mwaka 2003.

Tarehe 26 ya mwaka huo Cameroon walicheza nusu fainali dhidi ya Colombia na tuliisubiri kwa hamu kubwa kuona ni nini Waaafrika wenzetu wanakwenda kufanya katika nusu fainali hiyo iliyopigwa uwanja wa Stade De Gerland mjini Lyon.

Dakika ya 72 zikiwa zimesalia 18 mchezo uishe, Marc Vivien Foe alianguka katika eneo lake kipenzi analopenda kucheza uwanjani ilikuwa ni katikati ya uwanja na sio Afrika tu bali dunia nzima ikashikwa na mshituko kujiuliza ni nini kimetokea.

Foe alitolewa nje kwa machela akiwa anajaribu kuwekewa hewa ya Oxygen lakini baadae wingu zito likatanda barani Afrika kukaja simanzi kilio na majonzi baada ya taarifa kuenea kwamba shujaa wetu Vivien Foe ametutoka.

Foe alifariki kutokana na matatizo ya moyo huku mke wake akisema alikuwa akiumwa hata kabla ya mchezo lakini hakutaka kukaa nje bali alitamani kuivusha Cameroon kwenda fainali na alitaka kucheza katika mji aliokulia wa Lyon.

Kocha wa Cameroon kwa kipindi hicho Winfried Schafer alisema Foe hakuwa fiti na ndio maana hata mchezo na Marekani hakumpanga na katika mchezo dhidi ya Colombia alitaka kumtoa lakini kabla ya kufanya hivyo ndipo mauti yalimkuta.

Hii leo imepita miaka 10 toka tukio la Vivien Foe lipite na toka afariki Cameroon hawajawahi kushiriki michuano ya Confedaration Cup ambapo leo ni mara yao ya kwanza kupeperusha bendera ya nchi yao katika michuano hiyo tangu Foe alipofariki.

Arnaud Djoum ni mchezaji ambaye leo ataingia na mzigo mkubwa sana ameubeba mgongoni mwake kwani amevalishwa jezi aliyokuwa akiitumia Foe namba 17 na itamlazimu kuibeba sana Cameroon kama alivyofanya Foe katika michuano hiyo.

Djoum aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu Foe na akasema “tunataka kucheza kwa ajili yake na tumekuja hapa kwa ajili yake, ni heshima kubwa aliyotufanyia sisi kama Wacameroon” alisema Djoum kuelekea mchezo dhidi ya Chile..

Lakini sio tu Waafrika leo tutakaoishangilia Cameroon bali hata mashabiki wa Man City wanaweza ishangilia Cameroon wakikumbuka kwamba Foe ndio alifunga goli la mwisho la Man City wakati wakitumia uwanja wa Main Rode Stadium.

Achilia mbali mchezo kati ya Cameroon na Chile lakini pia mchezo mwingine wa kukata na shoka utapigwa hii leo ambapo Portugal wataikaribisha Mexico.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here