Home Kitaifa Imefungwa hat-trick ya kwanza Ndondo Cup 2017

Imefungwa hat-trick ya kwanza Ndondo Cup 2017

5918
0
SHARE

Hat-trick ya kwanza imefungwa leo Juni 18, 2017 kwenye michuano ya Ndondo Cup baada ya mshambuliaji wa Misosi FC kupiga bao tano peke yake na kuisaidia timu yake kupata pointi tatu dhidi ya Buguruni United ambapo mchezo huo ulimalika kwa matokeo ya Misosi FC 5-2 Buguruni United.

Watoto wa Buguruni United walianza kupata mabao yao mawili ya haraka kipindi cha kwanza hadi mapumziko Misosi walikuwa nyuma kwa Buguruni waliokuwa wakioza kwa magoli 2-1.

Kipindi cha pili Misosi wakaanza kufanya kweli na kufanikiwa kusawazisha kisha kuongeza magoli mengine matatu na kuibuka na ushindi. Mfungaji wa magoli ya Misosi Idd Selemani ‘Ronaldo’ akiwa kwenye kiwango bora kilichomavutia kila mtazamaji alieshuhudia mechi hiyo.

Magoli ya Buguruni United yamefungwa na Sultan Kasikasi dakika ya 20 na 32 (kwa mkwaju wa penati) wakati Ronaldo alipasia kamba dakika ya 34, 50 (kwa penati), 61, 82 na 90+3.

Michuano ya Ndondo Cup 2017 itaendelea tena kesho Jumatatu Juni 19, 2017 kwa mechi mbili ambapo Keko Faniture watacheza dhidi ya Black Six kwenye uwanja wa Tandika Mabatini na Mlalakuwa Rangers wao watakipiga na FC Goroka kwenye uwanja wa Mwl. Nyerere.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here