Home Kimataifa Wenyeji Russia waanza vyema michuano ya Confedaration Cup

Wenyeji Russia waanza vyema michuano ya Confedaration Cup

1734
0
SHARE

Kabla sijakupa habari kuhusu mechi yenyewe napenda kukujulisha kwamba mechi zote za Confederation Cup zinaonekana kupitia king’amuzi cha Startimes. Hakikisha unajiunga na Startimes au unalipia kifurushi kuanzia cha Mambo kuangalia michuano hii.

Leo michuano ya mabara almaarufu kama Confedaration Cup imeanza kupigwa pale nchini Urusi ambapo wenyeji wa michuano hiyo timu ya taifa ya Urusi waliwakaribisha NewZealand.

Urusi wamefanikiwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuwachapa NewZealand kwa mabao mawili kwa nunge na hivyo kukaa kileleni mwa kundi A.

Mchezo huo ulianza kutoa mabao dakika ya 31 tu ambapo NewZealand walijifunga wenyewe bao kupitia kwa Michael Boxall na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko huku Urussi wakiongoza kwa bao hilo moja.

Kipindi cha pili Warusi tena waliokuwa wakishangiliwa sana na mashabiki wao walifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 69 kupitia kwa Fredor Slomov na mchezo huo kumalizika kwa Urusi kuibuka na ushindi wa mabao hayo mawili.

Leo kutapigwa michezo miwili ambapo mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Ureno watacheza dhidi ya Mexico huku wawakilishi wa Waafrika timu ya taifa ya Cameroon wakiikabili Chile.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here