Home Dauda TV Video: Vituko vya mashabiki nje ya uwanja kwenye uzinduzi wa Ndondo Cup...

Video: Vituko vya mashabiki nje ya uwanja kwenye uzinduzi wa Ndondo Cup 2017

3547
0
SHARE

Tamu ya Ndondo Cup sio tu soka safi linaooneshwa uwanjani na wachezaji wa timu tofauti, bali burudani ya kutosha inapatikana pia nje ya uwanja ambapo mashabiki wanaokwenda kuzishuhudia timu zao huwa kiburudisho kwa wengine.

Kwenye mechi ya ufunguzi wa Ndondo Cup 2017 Makuburi SC vs Stim Tosha FC kuna jamaa wawili walikonga mashabiki wengi waliohudhuria mechi hiyo. Babu wa Stim Tosha alikuwa uwanjani akiongoza kamati ya ufundi kuhakikisha chama lake linaibuka na ushindi lakini haikuwa hivyo baada ya kubanwa na kulazimisha suluhu na Makuburi SC.

Kwa upande wa Makuburi wao walikuwa na Dulla Dibwangu ‘Mtoto wa mama Ndekule’ yeye amesema waliingia kwa imani lakini imani yao ikageuka na kuwa ‘Imani Madega’ kutokana na kuzidiwa kwa uchawi na Stim Tosha kwa hiyo game ijayo ameahidi na yeye atafanya maarifa ya kwenda kwa babu kusaka ushindi.

Hii hapa video unaweza kuangalia jinsi mashabiki hawa walivyo piga story na Dauda TV kwa nyakati tofauti.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here