Home Kitaifa Singida United wameinasa saini ya mfungaji bora wa Rwanda

Singida United wameinasa saini ya mfungaji bora wa Rwanda

6376
0
SHARE

Klabu ya Singida United imekamisha kumsainisha mkataba mshambuliaji Danny Usengimana ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda.

Usengimana amesaini mkata wa miaka miwili kucheza kwenye kikosi cha Singida United ambacho msimu ujao kitarejea ligi kuu Tanzania bara baada ya kufanikiwa kupanda ikiwa ni baada ya kusota kwa zaidi ya miaka 10 kikipambana kurejea VPL.

Mchezaji huyo pia aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Rwanda mara mbili mfululizo, msimu uliopita alifanikiwa kutupia kambani jumla ya mabao 19 akiwa na timu ya Polisi FC ya nchini Rwanda.

Mkurugenzi wa Singida United Festus Sanga amethibisha kumsainisha Usengimana mkataba wa miaka miwili kuitumika timu hiyo.

April 10, 2017 www.shaffihdauda.co.tz ilitoa story kuhusu tetesi za Singida United kutaka kumsajili Usengimana hivyo sasa si tetesi tena baada ya Singida United kukamilisha kusaini mkataba na nyota huyo wa Rwanda na klabu kuthibisha rasmi kwamba ataitumikia timu yao kuanzania msimu ujao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here