Home Kimataifa Raisi wa Real Madrid akiri uwezekano wa Cr7 kurudi Manchester United

Raisi wa Real Madrid akiri uwezekano wa Cr7 kurudi Manchester United

8125
0
SHARE

Ronaldo hataki ujinga hata kidogo, hivyo ndio unaweza kusema kwani mwanasoka bora huyo wa dunia kitendo cha kuandamwa tu siku moja na vyombo vya sheria vya nchini Hispania kesho yake ametishia kuondoka na anasema hataki tena kukaa katika nchi hiyo.

Swali likaja, Je akiondoka Hispania ni wapi anakwenda? swali ambalo jibu lake ni rahisi sana kwani hakuna mahala Ronaldo anapafurahia na kupamiss kama jiji la Manchester kufanya mazoezi katika uwanja wa Carrington na kucheza mechi za nyumbani katika dimba la Old Trafford hiyo ni kati ya furaha yake.

Tayari aliposema tu anataka kuondoka vyombo vya habari vimeshaanza kuandika uwezekano wa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kurudi kuichezea Manchester United ambako anatamani kumaliza maisha yake ya soka katika klabu hiyo iliyomtambulisha ulimwenguni.

Ramon Calderon ni raisi wa zamani wa Real Madrid na kwa uzoefu wake wa soka na kuishi na wanamichezo wakubwa dunia amekiri kwamba pamoja na uwezo wa kifedha wa Real Madrid lakini ni ngumu kumzuia Ronaldo kurudi United kama akitaka kurudi na atabaki Madrid kama akitaka pia.

Calderon ndiye raisi aliyemleta Ronaldo Real Madrid na ndiye alimuuza Robinho kwenda Man City na anasema anajua Ronaldo alivyo akiwa anataka kitu anachokipenda na kukiri Ronaldo aliondoka United baada ya kushinda kila kitu lakini moyo wake uko Old Trafford.

“Wakati najaribu kumnunua ilikuwa kama hivhivi alikuwa anataka kuja na hakuwaficha United aliwaambia anataka kuondoka na hicho ndio kinaenda kuwatokea Real Madrid kwa sasa na inapofika hatua hiyo kama raisi unabaki huna la kufanya zaidi ya kumuacha aende kama nilivyofanya kwa Robinho” alisema Calderon.

Calderon alisema hana uhakika kama kweli Ronaldo amesema anataka kurudi United lakini kama ni kweli atarudi tu hata kama uhusiano wake na Mourinho sio mzuri lakini hiyo haitamzuia yeye kurudi katika klabu ambayo anaipenda na ameshinda mataji akiwa nayo.

Nguvu ya kipesa waliyonayo Manchester United pamoja na uwepo wa kocha Alex Ferguson katika majukwaa ya klabu hiyo kila inapocheza vinamuaminisha Calderon kwamba Ronaldo anaweza kurudi Manchester United na hata kama sio hapo ila hataondoka nje ya bara la Ulaya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here