Home Kimataifa Moto wa Confedarations Cup kuanza kuwaka hii leo.

Moto wa Confedarations Cup kuanza kuwaka hii leo.

3290
0
SHARE

Michuano ya mabara almaarufu kama Confedaration Cup inaanza kutimua vumbi nchini Russia hii leo kwa wenyeji Russia watakaoikaribisha New Zealand katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo.

Mchezo huu kati ya Russia na NewZealand unatarajiwa kupigwa katika dimba la St Petersburg uwanja wa nyumbani wa klabu ya St Petersburg huku Winston Reid mlinzi wa West Ham na timu ya taifa ya New Zealand akikosa mechi hiyo kutokana na majeraha.

Timu ya taifa ya Ureno wataliwakilisha bara la Ulaya kama mabingwa wa bara hilo huku waandishi wa habari wakiwa wamepiga kambi katika timu hiyo kufuatilia mkasa mkubwa wa kodi unaomuandama Cristiano Ronaldo.

Andre Silva mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno amewaambia waandishi wa habari kwamba “Ronaldo anaichukulia michuano hii serious sana na hawazi yanayotokea nje ya uwanja bali akili yake yote iko katika michuano hii”

Toka suala la Ronaldo kudaiwa kukwepa kodi lianze kutawala vyombo vya habari inasemekana Mreno huyo hana raha na anafikiria kuondoka nchini Hispania, Ureno wenyewe watakuwa uwanjani kesho Jumapili kucheza dhidi ya Mexico.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here