Home Kitaifa Mambo 5 yatakayokuvutia mechi ya ufunguzi Ndondo Cup 2017 Makuburi SC vs...

Mambo 5 yatakayokuvutia mechi ya ufunguzi Ndondo Cup 2017 Makuburi SC vs Stim Tosha

3601
0
SHARE

Leo Juni 17, 2017 ndio ile siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa na wapenzi wa michuano ya Ndondo Cup, leo utapigwa mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi kwa msimu huu mpya ukiwa ni msimu wan ne tangu kuanzishwa kwa mashindano haya.

Ukiachana na mambo mengine yote, game ya leo si ya kukosa si kwa sababu tu ni ya ufunguzi ila ukali na ugumu wa mechi yenyewe ndio unaifanya mechi hii kuwa tamu nay a kuvutia machoni mwa watu wa Ndondo.

Game itakuwa ni kati ya Stim Tosha kutoka pande za Mabibo Sokoni-Mahakama ya Ndizidhidi ya Makuburi SC watoto wa Tabata jamani leo kazi ipo.

Harufu ya ligi kuu hii hapa

Picha linaanza timu zote zina watu wanaokipiga ligi kuu Tanzania bara, Makuburi wana golikipa wa Mwadui FC Shabani Kado mshindi wa zamani wa tuzo ya golikipa bora wa VPL huku akiwa amewahi kuidakia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ sasa leo atakuwa kwenye goli la timu yake ya kitaa kuwakilisha kwenye Ndondo.

Shabani Kado

Upande wa pili Stim Tosha kuna Kelvin Sabato ‘ Kiduku’ mchezaji wa Majimaji FC ya Songea lakini kwa tetesi za usajili wa kipindi hiki anahusishwa kuwa kwenye radar za Simba, sasa leo ataonesha kwamba kwa nini atahusishwa kuwa kwenye darubini za Simba.

Kelvin Sabato ‘Kiduku’

Huku pia yupo Thomas Morris nyota wa zamani wa mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara (Young Africans SC) licha ya ukongwe lakini bado yupoyupo sana kwenye soka Mbwiga anamsemo wake kuwa ‘ukijua umejua, ujuzi hauzeeki.’

Kiduku vs Kado

Hawa jamaa wawili ni kivutio kingine tena kwenye game ya leo. Waliwahi kucheza timu moja wakati huo Kiduku akiwa Madui kabla ya kuhamia Stand United kisha Majimaji. Kiduku ni mshambuliaji, Kado golikipa kwa hiyo Kiduku atakuwa akitafuta kumtungua Kado wakati huo Kado atakuwa akizuia mashuti ya Kiduku yasikuse nyavu zake, patamu hapo.

Nyange la nje

Jana nilipotembelea maskani ya timu zote mbili, mashabiki walikuwa na nyimbo zao maalum kwa ajili ya game ya leo. Mashabiki wa Stim Tosha wanasema ‘waje hata sasa hivi hao maboya’ wakati watoto wa Tabata wao wanawimbo wao unasema ‘usela ukizidi sana mwishowe utalala jela’ wakidai kwamba watoto wa Mabibo wanajidai wao ni wahuni wa kupindukia.

Hamasa

Hii game ujue sio ya kitoto kila timu imejipanga kuchukua pointi tatu muhimu za kuanza nazo kwenye mbio za kuwania kufuzu hatua mtoano (16 bora) sasa hapa kwenye hamasa ndio utamu mwingine ulipo wa game hii.

Mabibo (Sim Tosha) wamepanga kuhamia kwenye uwanja wa Kinesi kuipa support timu yao, kwa mujibu wa kiongozi wao hadi jana saa saba mchana, tayari kuliwa na mashabiki zaidi ya 200 ambao wameshachanga pesa kwa ajili ya kununua tiketi za mchezo wa leo.

Nilipokuwa Tabata maskani ya Makuburi SC moja ya viongozi wa timu ile alinithibitishia kwamba wao kila goli litanunuliwa kwa T-shirt, raba au kiatu, Jeans pamoja na kanzu ikiwa ni maandalizi kwa mfungaji kuelekea sikukuu ya Idd mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ujirani

Hizi timu ni majirani na wana upinzani wao kulingana na maeneo wanayoishi. Mabibo na Tabata sio mbali sana, kwa wakazi wa Dar watakuwa wanaelewa ninaposema timu hizi ni majirani, kwa hiyo kila mmoja anataka kuja kutamba kwa mwenzake hususan baada ya kupata ushindi tena kwa kumfunga jirani yake.

Bifu lililopo hapa kwenye ujirani kwamba, Makuburi wanajitapa kuwa wao ni chuo cha soka kama ilivyo Mtibwa Sugar wazee wa kuibua vipaji hii inatokana na ukweli kuwa Stim Tosha huwa inachukua watoto wa Tabata na kuwapeleka Mabibo kucheza kwenye timu yao kwa hiyo Makuburi wao wanasema wanawachezaji wa kutosha kuliko Stim Tosha ambao hawana wachezaji wanasubiri kukwapua kutoka kwao. Kwa hiyo game ya leo ni Makuburi A vs Mabuburi B pale Kinesai.

Kwa wale ambao hawatoweza kufika uwanja wa Kinesi, Shekilango-Sinza, au mtazamaji wa mkoani mzigo utakuwa mubashara kupitia Azam TV kwa hiyo usikae mbali na TV yao utakosa mengi.

Hatuishi hapo tu, unaweza kufuatilia updates za kila wakati kupitia mitandao ya kijamii maalum kwa ajili ya Ndondo Cup. Instagram (ndondo_cup) ,Facebook (NdondoCup), Twitter (@NdondoCup) na Tovuti (www.ndondocup.co.tz) kote huko kutakuwa na madini ya Ndondo Cup 2017.

Ndondo Cup 2017 tunasema Waleteee…

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here