Home Kitaifa Makuburi, Stim Tosha wameizindua Ndondo Cup kwa sare

Makuburi, Stim Tosha wameizindua Ndondo Cup kwa sare

3909
0
SHARE

Game ya ufunguzi ya hatua ya makundi michuano ya Ndondo Cup 2017 Makuburi SC vs Stim Tosha imemalizika kwa suluhu na timu hizo kugawana pointi moja moja.

Pambano lilikuwa kali huku kila timu ikipambana kupata goli ili kuchomoka na pointi tatu kwenye mechi ya kwanza na kujiweka kwenye mazingira mazuri katika Kundi G.

Si Kelvin Sabato ‘Kiduku’ wala Paul Maona, wachezaji hao walibanwa vilivyo na wapinzani wao na kushindwa kuzifungia timu zao. Licha ya nafasi kadhaa za kufunga lakini uimara wa mabeki na walinda milango ulisaidia kuziponya nyavu zao.

Mashabiki wameonesha muamko mkubwa kwa kujitokeza kwenye uwanja wa Kinesi kwa ajili ya kushuhudia pambano hilo ambapo kulikua na burudani kibao kutoka kwa wasanii wa muziki wa Kisingeli (Sholo Mwamba, Man Fongo pamoja na Moto Kombati ‘mwendo wa mateka’.

Kikubwa baada ya mchuano huo ni ustaarabu ulionesha na mashabiki wote walihuhuria mechi kuondoka uwanjani kwa ustaarabu wa hali ya juu kama tofauti na wengi ambao wamekua wakiamini Ndondo ni sehemu ya fujo na vurugu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here