Home Kimataifa Kocha wa Mexico atoa onyo kwa wachezaji wake kuhusu Ureno.

Kocha wa Mexico atoa onyo kwa wachezaji wake kuhusu Ureno.

2798
0
SHARE


Baada ya hapo jana kupigwa mchezo wa ufunguzi wa michuano ya mabara kati ya Urusi na Newzealand, leo kutapigwa mchezo mwingine ambapo Ureno watakuwa dimbani dhidi ya Mexico.

Ureno wakiwa na mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo wanaonekana tishio sana kutokana na timu yao kujaa vipaji vingi vya wakongwe na vijana ambapo wameleta mseto fulani wakuogopesha.

Walinzi wa Mexico wanaweza kuingia uwanjani hii leo wakielekeza nguvu zao kumzuia Cristiano Ronaldo asifunge lakini jambo hilo linaonekana linaweza kuwa hatari kwa Mexico kama wakifanya hivyo.

Kocha wa Mexico Juan Carlos Osorio amewaambia wachezaji wake kwamba waizuie Ureno kama timu na waache kuhangaika na mchezaji mmoja tu akimaanisha Cristiano Ronaldo.

“Cristiano Ronaldo ni hatari lakini ukiangalia yupo mtu kama Nani,Quaresma au Gelson Martin na wote hao ni hatari hatupaswi kumzuia Ronaldo tu” alisema Juan Osorio.

Osorio pia hakusita kuelezea woga wake kwani kundi B walilopo linaonekana kundi la kifo zaidi na wao ndio wanaoonekana wasindikizaji katika kundi hilo kutokana na vigogo waliopo lakini akaahidi watapambana.

Kundi B la michuano hiyo ipo timu ya taifa ya Mexico, wapo mabingwa wa Ulaya timu ya Ureno, wapo mabingwa wa dunia Ujerumani na mabingwa wa Copa America timu ya taifa ya Chile.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here