Home Kitaifa Jonas Mkude, Simba, wamalizana

Jonas Mkude, Simba, wamalizana

14120
0
SHARE

Kiungo na nahodha wa Simba Jonas Mkude ameongeza mkataba wa miaka miwili (2) kuendelea kubaki Msimbazi baada ya awali kuwa na mvutano mkubwa kati ya uongozi na Mkude juu mkataba mpya kufuatia wa awali kuelekea ukingoni.

Mkude alikuwa anahusishwa kuhamia Yanga kutokana na mvutano wa kimaslahi uliokuwepo kati yake ya viongozi wa Simba. Yanga pia walikuwa wanafanya kila linalowezekana ili kuinasa saini ya mchezaji huyo, taarifa ambazo si rasmi zinadai Yanga walikuwa tayari kutoa kiasi kikubwa cha pesa pamoja na gari ya kutembelea kwa ajili ya kumnasa Mkude.

Baada ya mashabiki wa Simba kuwa matumbo joto kwa muda mrefu kuhusu hatma ya Mkude ndani ya Simba, hatimaye furaha imerejea miongoni mwao ukizingatia tayari mshambuliji wa timu hiyo Ibrahim Ajib ameshamalizana na wakali wa Jangwania Yanga.

Taarifa za ndani ya uongozi wa Simba zinasema kuwa, pande mbili (Jonas Mkude na uongozi wa Simba) zimefikia makubaliano na kuridhiana masharti yote kabla ya Mkude kusaini mkaba wa kuendelea kubaki Msimbazi kuitumikia Simba kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here