Home Kitaifa Shabani Kado amesaini Makuburi SC Ndondo Cup 2017

Shabani Kado amesaini Makuburi SC Ndondo Cup 2017

5992
0
SHARE
Shabani Kado

Golikipa wa Mwadui FC ya ligi kuu Tanzania bara Shabani Kado, amesajiliwa na Makuburi SC kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwenye michuano ya Ndondo Cup iatakayoanza rasmi kesho kwa hatua ya makundi.

Kado amesaini mkataba leo mbele ya viongozi wa Makuburi SC na kukabidhiwa jezi yake yenye namba moja mgongoni tayari kabisa kwa ajili ya kuiongoza Makuburi kwenye michuano ya Ndondo Cup msimu huu 2017.

Zoezi hilo limefanyika maeneo ya Tabata Makuburi ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabisa kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi. Ikumbukwe Kado ni golikipa mwenye uzoefu kwenye mpira wa Tanzania akiwa amewahi kushinda tuzo ya golikipa bora wa ligi kuu Tanzania bara pamoja na kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Kado amesema ameamua kujiunga na Makuburi SC kwa sababu ndio sehemu anayoishi kwa hiyo anawaunga mkono viaja wa mtaani kwao.

“Mimi ni mkazi wa maeneo haya ni sehemu ambayo nimekulia, wachezaji wengi wa timu hii nimekuwa nao hivyo nimeamua kujiunga na wenzagu kui-support timu ya nyumbani” – Kado.

Kado atakuwa goli kesho Jumamosi kwenye mechi ya ufunguzi wa Ndondo Cup 2017 hatua ya makundi ambapo Makuburi SC itakuwa ikicheza dhidi ya Stim Tosha kwenye uwanja wa Kinesi pale Shekilango jijini Dar es Salaam.

Ukiachana na Kado, Makuburi SC pia imetambulisha wachezaji wake wengine ambao itawatumia katika msimu huu wa Ndondo Cup 2017.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here